AKIJA, MKURUGENZI WA KETRACO ATASHINDA WOTE UGAVANA 2022.
Makala ya Mhariri Charles Shiundu. Iwapo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la usambazaji umeme la humu nchini KETRACO Bw. Fernandes Barasa atazamia kuwania kiti kama Gavana wa Kakamega mwaka wa 2022, uwezekano ni mkubwa kwamba atawashinda wagombezi wote. Darubini inaonyesha kwamba, shirika la Kibinafsi Barasa Foundation limeimarisha utenda kazi mashinani mwa kaunti ya Kakamega na miradi ya manufaa kwa wananchi wa kawaida. PIKIPIKI Kwanza, shirika hilo limezamia uchumi wa vijana kwa kuwapa pikipiki kwa malipo ya chini zaidi kila siku sita kwenye wiki la siku saba. Vijana kuanzia Lugari hadi Khwisero wameweza kujimudu angaa ki uchumi kwa mkopo rahisi wa pikipiki hizo ambazo zimesambazwa kote. Kulingana na muktadha, uchumi wa magharibi umeimarika mara dufu na wengi wa vilama hao wameweza kwa kiasi angaa kidogo kuepuka na mihemko ya ki uchumi kufwatia mlipuko wa Ugonjwa wa Covid-19 nchini Kenya mwezi wa tatu Mwaka huu. Savey uliofanywa inaonyesha ya kwamba kwenye kila...