AKIJA, MKURUGENZI WA KETRACO ATASHINDA WOTE UGAVANA 2022.



Makala ya Mhariri Charles Shiundu.




Iwapo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la usambazaji umeme la humu nchini KETRACO Bw. Fernandes Barasa atazamia kuwania kiti kama Gavana wa Kakamega mwaka wa 2022, uwezekano ni mkubwa kwamba atawashinda wagombezi wote.

Darubini inaonyesha kwamba, shirika la Kibinafsi Barasa Foundation limeimarisha utenda kazi mashinani mwa kaunti ya Kakamega na miradi ya manufaa kwa wananchi wa kawaida.

PIKIPIKI

Kwanza, shirika hilo limezamia uchumi wa vijana kwa kuwapa pikipiki kwa malipo ya chini zaidi kila siku sita kwenye wiki la siku saba. 

Vijana kuanzia Lugari hadi Khwisero wameweza kujimudu angaa ki uchumi kwa mkopo rahisi wa pikipiki hizo ambazo zimesambazwa kote. 

Kulingana na muktadha, uchumi wa magharibi umeimarika mara dufu na wengi wa vilama hao wameweza kwa kiasi angaa kidogo kuepuka na mihemko ya ki uchumi kufwatia mlipuko wa Ugonjwa wa Covid-19 nchini Kenya mwezi wa tatu Mwaka huu. 

Savey uliofanywa inaonyesha ya kwamba kwenye kila kitongoji, waliofaidika na mkopo wa pikipiki wamemudu hali zao kushinda hali ilivyokuwa hapo awali. 

SODO.

Mradi mwingine wenye shime Magharibi mwa Kenya ni ule wa kuwapa wasichana waliobalehe sodo kujikimu kwa hedhi za kila mwezi. 

Miongoni mwa vikundi vilivyo faidika na sodo ni Shule za Msingi, makundi ya akina mama na makundi ya watu binafsi, kawaida, ukosefu wa sodo wakati wa hedhi umechangia wasishana wengi kuwacha shule au kumudu aibu kila mwezi. 

Shirika hili la Baraza Foundation, kulingana na walimu wakuu wa shule zilizo faidi limeongeza idadi ya wanafunzi shuleni yaani (retention) kwa msaada wa sodo takriban miaka miwili sasa. 

UJENZI WA MAKAO

Zaidi ya watu mia tatu 300 wamefaidika na mradi wa ujenzi wa makao wa shirika hili, wengi wao wajane wamepata nyumba za mabati baada ya makao yao kubomolewa katika hali tataninshi. 

Kulingana na Martha Shiundu, mjane wa miaka sabini na mbili, ujenzi wa nyumba kwake ni jambo la muhimu sana kwa kua baada ya mafuriko ya mwezi wa pili, khamsa yake ilisikika na shirika hili na hivi sasa ana makao mapya. 

Kulingana na daktari Sammy Ambani kwenye Hospitali ya kaunti kule Matungu, wajane wengi wamepoteza maisha sehemu hio kwa ugonjwa wa Malaria unaoletwa na mbu kwa kulala njee kukosa makao. 

Dk Ambani amesema kuimarisha makao kwa wakaazi ni jambo la muhimu  hasa wakati huu ambao misimu ya baridi imekua mingi. 

Mradu huu wa Makao umeenea Matungu, Butere na khwisero na kulingana na Meneja kwenye shirika hili mwanzo wa mwaka, mradi utaenea kote kaunti ya Kakamega. 

SOKA

Mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 kote nchini ulisababisha kufungwa kwa shule nchini ndio maana Barasa Foundation lilianzisha ligi ya mpira wa miguu kwenye Mashinani yote kaunti ya Kakamega.

Wazo hili lilikuja wakati ambapo wazazi wengi walilalamika ya kwamba vijana wao wamekua bila la kufanya na wamejiingiza kwenye utumizi wa mihadarati.

Shirika hili lisilo la kujifaidisha lilianzisha mechi kwenye timu zaidi ya 30 kote Kakamega ambapo mshindi ataibuka na kitita cha shilingi milioni moja hadi elfuia mbili mwisho ni mwa mwaka huu.

Kulingana na watafiti hata Gavana anayeondoka Whycliffe Oparanya alupowania kiti hiki hakuna na miradi ya Mashinani ya kukuza uchumi wa mwananchi mdogo. 

Wadadisi wanasema ya kwamba, ikiwa Mkurugenzi huyu wa kuheshimika kimataifa ataamua kuwania kiti cha Ugavana kwenye chama cha kisiasa chochote, atashinda uchaguzi huo mapema sana.
Mwisho. 
Baadhi ya makundi ya kibinafsi yanayo faidika na Sodo za shirika la Barasa foundation likiongozwa na Jannet Barasa.

Makao ya Mjane kule Matungu kabla ya shirika kuingilia na kujenga nyumba ya kisasa (Chini).



UJUMBE: Makala haya yamesanifishwa na Mwandishi wa Habari Huru Bw. Joel Eshikumo. 

Comments

Popular posts from this blog

UNMASKING MOFFAT MANDELA OPARANYA'S POCKET PUPPET.

VIDEO: HOW MUMIAS CID BOSS ROBBED KAKAMEGA SENATOR OFF KSH 2M